![]() |
||
|
Mwamba house sio tu tumenuia au panga kusaidia watoto yatima na watoto wa mitaani pia tutaendesha vipindi vya masomo kwa watoto wa kawaida yaani wasio yatima, zahanati, makundi ya ushauri kwa waathirika wa ukimwi wamaume, wanawake, watoto na elimu jinsia hapa tutakuwa tunawafundisha wanajamii wa Mahina kuhusiana na maradhi ya zinaa: ugonjwa wowote unaoambukizwa kwa njia ya jimai au zinaa na elimu ya ufundi. Tunaamini ya kwamba kwa kuelimisha na kusaidia familia zinazoishi katika mazingira magumu,tunaweza kutoa ustadi muhimu ambao utawasaidia kuboresha kiwango cha maisha yao ya sasa na ya baadaye. Mwanza inapatilkana katika pwani ya Ziwa Victoria, itakuchukua saa moja na nusu kwa usafiri wa anga kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza. Fedha inayotumika ni Shillingi ya Kitanzania, na Dola moja ya Kimarekani ni karibu sawa na shillingi elfu moja na mia mbili (1200) ya Kitanzania.
|
||