Mwaka 2007, kundi la wanaume na wanawake kutoka Tanzania, Australia na Canada waliona haja ya kuongeza ongezeko la huduma na nyenzo kwa ajili ya mayatima, watoto wa mitaani na jamii nzima ya Mwanza, Tanzania.

Baada ya mkutano wa mashauriano ya kina na nyumba za mayatima yaani (orphanages) na vituo vingine vya kulea watoto, serikari na viongozi wa serikari za mitaa, eneo la Mahina mkoani Mwanza lilichaguliwa au teuliwa kwa ajili ya kuanzisha au kuimarisha nyumba ya watoto yatima yaani (orphanage) na pia kituo cha elimu ya wanajaamii wa Mahina.

Shabaha yetu ni kupata kiwanja Mahina, na kujenga mabweni yetu ndani ya miezi michache ijayo. Tukiwa tunasubili kupata fedha za kutosha kununua eneo Mahina, kwa sasa madarasa ya wanajamii yanaendelea kwa watoto wa mahina na tunajitaidi kupokea au kukutana na mahitaji yao ya msingi kama chakula na maji.

Waanzilishi wa Mwamba house wana uzoefu mkubwa kufanya kazi na watoto yatima na watoto waishio katika mazingira magumu au hatarishi mkoani Mwanza, na tunaajiri Watanzania na watu kutoka nchi mbalimbali dunia kote.Tutakuwa tunawakaribisha watu wajitoleao kwa hiari yaani (volunteers) kuja kutusaidia katika mradi wetu kuanzia Mwezi wa nane mwaka huu wa 2007.

Tunasubili kusajiriwa na serikari ya Tanzania kama NGO, tunatazamia usajiri utatolewa hivi karibuni.