Tunatambua ya kuwa kuna watu wengi ambao wanatamani kutusaidia lakini hawawezi kusafiri kuja Tanzania. Utaratibu wetu wa kuwasaidia watoto ukiwa nyumbani unaruhusu watu duniani kote kuunga mkono juhudi zetu mkoani mwanza kwa kufanya matukio ya kuchangia, kukusanya vifaa kama vile nguo, madaftari ya mzoezi, kalamu, vifaa vya michezo, dhana, compyuta, vitabu na vifaa vya kufundishia kwa ajili ya matumizi ya Mwamba House.

Tutakuwa tunawatumia marafiki zetu Barua au taarifa kupitia njia ya compyuta (email), yaani barua pepe zinazo husiana na utaratibu wetu wa kuwasaidia watoto ukiwa nyumbani mara kwa mara itakujulisha maendeleo yanayofanyika Mwamba House, ili kwamba uweze kuona msaada wako unavyofanya tofauti kwa watoto wetu!

Watu ambao wako tayari kujiunga katika utaratibu wetu wa kuwasadia watoto ukiwa nyumbani wanaweza kuwasiliana nasi kupitia njia ya (email) yaani barua pepe, zinazopatiakana katika ukrasa wetu wa mawasiliano.